Kulingana na shirika la habari la Abna, likinukuu Al Mayadeen, utawala vamizi wa Kizayuni uliingia katika eneo la Kroum al-Marah huko Meiss al-Jabal na kulipua nyumba ya makazi katika eneo hilo.
Jana pia, katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon, watu wawili waliuawa (walishahidika) na wengine saba walijeruhiwa. Kulingana na Wizara ya Afya ya Lebanon, droni za Kizayuni jana zililenga gari la raia katika mji wa Al-Duwair Kusini, na kusababisha kifo cha raia mmoja na kujeruhiwa kwa wengine saba.
Shambulio hilo lilisababisha moto mkubwa kwenye eneo hilo, ambao ulihusisha magari kadhaa na kuharibu nyumba na maduka ya jirani.
Katika shambulio la wakati mmoja, droni ya Kizayuni pia ililenga pikipiki katika mji wa mpakani wa Aita al-Shaab, na kusababisha kifo cha raia mwingine.
Mashambulizi haya yanafanyika katika mfumo wa ongezeko hatari la uchokozi wa utawala vamizi wa Israel katika maeneo ya Kusini, huku raia na miundombinu wakilengwa mara kwa mara, na kwa sababu ya kuendelea kwa uvunjaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel.
Jana pia, maeneo ya mashamba ya Bastara na eneo la Azrail karibu na mji wa Kafr Shuba yalishambuliwa kwa risasi na maguruneti kutoka kwa vituo vya vikosi vya adui vya Israel vilivyoko Al-Ramtha.
Your Comment